Fanikisha Harusi Yako Remotely Popote Ulipo: RedPoint Yaonyesha Mfano Iringa

Hivi karibuni, RedPoint imetekeleza kwa mafanikio harusi ya Bwana Mfimwi na Bi Alice iliyofanyika tarehe 12 Julai 2025, Iringa.
Hadithi hii inaonyesha jinsi teknolojia inavyoweza kurahisisha sherehe zako popote ulipo, huku RedPoint ikikupa utulivu wa akili na mpangilio bora bila stress.
Jinsi Bwana Mfimwi Alivyotupata na Harusi Ilivyopangwa
Bwana Mfimwi alitupata kupitia Google alipokuwa akitafuta njia rahisi ya kuratibu harusi yao ya ndoto.
Baada ya kusoma huduma zetu kupitia tovuti yetu, alijisajili haraka na kulipia huduma kupitia malipo ya mtandaoni, bila haja ya kusafiri Dar es Salaam au ofisini kwetu.
Timu ya RedPoint ilianza mara moja kufanya kazi naye kupanga sherehe kwa karibu kwa njia ya simu na WhatsApp.
✅ Tulimsaidia kutengeneza e-Card zenye jina la kila mgeni na QR Code
✅ Tulituma mialiko kwa WhatsApp na SMS, huku tukiwapigia simu waalikwa wote
✅ Tulifuatilia wageni waliopokea na waliothibitisha kuhudhuria ili kurahisisha maandalizi
Mafunzo kwa Kamati ya Harusi
Ili kuhakikisha mchakato unakwenda kwa urahisi siku ya tukio, RedPoint ilifanya mafunzo kwa wajumbe wawili wa kamati ya harusi kuhusu jinsi ya kutumia simu zao kuscan QR Code za waalikwa wanapofika kwenye eneo la tukio.
Hii ilirahisisha kuhesabu wageni waliofika na kudhibiti idadi ya viti, chakula na mpangilio wa wageni kwa urahisi mkubwa.
Kwa Nini RedPoint Ni Msaidizi Bora Kwenye Sherehe Yako?
✅ Huduma ya Haraka na Rafiki – Tunashirikiana nawe bila kujali uko mkoa gani, kwa kutumia simu, WhatsApp na email.
✅ Teknolojia Rahisi – Wageni wako wanaalikwa kwa urahisi, wanapata ramani ya eneo, na wanapokelewa kwa heshima siku ya tukio.
✅ Kuokoa Muda na Gharama – Huna haja ya kuchapisha kadi nyingi au kuzunguka kutoa mialiko, kila kitu kinaenda kidigitali kwa ufanisi.
✅ Inafaa kwa Harusi, Send-Off, Kitchen Party na Sherehe za Kiofisi.
Shuhuda Kutoka Kwa Bwana Mfimwi
“Sikujua kama harusi inaweza kupangwa kwa urahisi hivi nikiwa Iringa. RedPoint imenisaidia sana kwa kunipa huduma za kidigitali, wageni wangu walifurahia sana na kila kitu kilienda kwa mpangilio. Asante RedPoint kwa huduma nzuri na za kisasa.”
Na Harusi Yako Je?
RedPoint ipo tayari kukusaidia kupanga harusi yako popote ulipo Tanzania, bila stress na kwa gharama unazoweza kumudu.
Tunahakikisha wageni wako wanapata mialiko kwa wakati, wanakumbushwa michango kwa heshima, na siku ya tukio kila kitu kinaenda kwa urahisi na kisasa.
Kadi hii ya Mwaliko ilibuniwa na bwana Mfimwi mwenyewe.
Wasiliana Nasi Leo:
📲 WhatsApp: 0767302952
🌐 Tovuti: https://rebpoint.co.tz
📧 Email: mambo@rebpoint.co.tz