Hongera Issack na Suzan! ππ

Weekend hii tulishuhudia sherehe ya harusi ya Issack na Suzan iliyofana sana pale Mirado Hall, Sinza Makaburini. Ilikuwa siku ya furaha, mapenzi na tabasamu, huku familia na marafiki wakikusanyika kusherehekea upendo wao.
Kama kawaida, redPoint tulikuwepo kuhakikisha wageni wanakaribishwa kwa utaratibu kupitia huduma zetu za kuscan kadi za mwaliko kwa ufanisi na urahisi. Wageni waliingia bila usumbufu, hali iliyowapa nafasi ya kufurahia sherehe badala ya kusubiri mistari mirefu.
Lakini harusi hii ilikuwa ya kipekee kwetu, kwani ni mara ya kwanza kwa Send-Off ya bi harusi mtarajiwa kutumia huduma za redPoint, kisha tukahudumia tena kwenye harusi yao. Hii imetupa furaha kubwa kuona wateja wetu wakiridhika na kurudi tena, huku tukishuhudia hatua nyingine kubwa katika maisha yao.
Tunawashukuru Issack na Suzan kwa kutupa nafasi hii, na tunawatakia ndoa yenye baraka, upendo na amani ya kudumu.
Unataka harusi yako iwe laini na yenye mpangilio?
redPoint tunakusaidia:
β
Kadi za mialiko za kidigitali zenye QR Code
β
Usimamizi wa wageni kwa kuscan mlangoni kwa haraka
β
Kumbukumbu za wageni waliokuja
β
Kadi za shukrani na usimamizi wa zawadi
π² Wasiliana nasi WhatsApp kwa maandalizi ya sherehe yako: 0767302952
redPoint – Scan. Smile. Celebrate.